BREAKING NEWS!!!! AJALI MABYA, MELI YAZAMA IKIWA INAELEKEA PEMBA WENGI WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA...!!!
Taarifa zilizo tufikia sasa zinasema kwamba meli ambayo imesadikika kuondoka Unguja kuelekea Pemba imezama, huku ikiwa imesheni abiria zaidi ya 500 wengi wao wakiwa ni wanafunzi ambao walikuwa wametoka rikizo ya Iddy, Mpaka sasa zaidi ya watu watano wamethibitika kuwa wamepoteza maisha, na wengine hawajapata msaada mpaka ilipo fika alfajiri. Hata hivyo baadhi ya abiria walio kuwa pembezoni mwa upande wa meli amboo haijazama walikuwa wanafanya jitihada za kupiga simu kupata msaada bila mafanikio. meli hiyo pia inasemekana ilikua imeshena mizigo na kuzidiwa .
Hadi hivi sasa taarifa ambazo zimetufikia ni kwamba Zanzibar imekumbwa na msiba mkubwa. Kwa kifupi hali ni hiyo lakini kwa maelezo zaidi tutarifiana muda mfupi kutoka sasa kama hizi habari ni za ukweli na hali ikoje huko Visiwani jitihada za kuokoa watu bado kutokana na mawasiliano .
LATEST UPDATE:
ABIRIA 250 WAOKOLEWA WAKIWA HAI KATIKA AJALI YA MELI YA SPICE ISLAND...!!!
Watu 250 wameokolewa wakiwa hai katika meli iliyozama ya Mv Spice Islanders iliyokuwa ikitokea Bandari ya Malindi Unguja kuelekea Bandari ya Wete Kisiwani Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Mohamed Aboud Mohamed amesema watu hao wameokolewa na Vikosi vya uokoaji na wananchi mbalimbali wanaotoa msaada wa uokozi katika tukio la kuzama kwa meli hiyo huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Waziri Aboud amesema watu hao wamesafirishwa kwa kutumia Boti zinazokwenda kasi za Zanzibar ambazo ilikwenda kutoa msaada katika eneo la tukio.
Amesema watu hao baada ya kufika Bandari ya Malindi Unguja watapelekwa Viwanja vya Maisara kwa ajili ya kuungana na familia na jamaa zao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein yupo katika eneo la tukio huko Nungwi ili kujionea hali halisi ya tukio hilo.
Comments
Post a Comment