Mh. Balozi Kapya akiningia na binti yake katika ofisis za Registry Reading
Bwana harusi akitia sahihi kwenye cheti cha ndoa
Picha ya pamoja na pande zote za familia pamoja na wadau wadau walishuhudia harusi hiyo
Pozi baada ya harusi
Bwana harusi Dello
Bwana na Bibi harusi wakiwa wanameremeta
Boat inayoitwa Caversham Princess ikiwasubiri maharusi tayari kwa sherehe
Maharusi wakipewa maelekezo kabla yakuingia kwenye boat
Dello akimlisha keki mkewe
Bonge la kiss
Mh. Balozi akitoa nasaha zake kwa bwana na bibi harusi
Mh. Balozi Kallaghe na Mh. Balozi Kapya wakibadilishana mawili matatu
Wadau wakijimwaga kwa raha zao
Wakati wakulisakata rumba
Zawadi maalum kutoka kwa Mzee Abdul Dello
Kila kitu kimekwenda poa na jiko nimeshavuta sasa tugange yajayo
****************************************************
****************************************************
Salam,
URBAN PULSE CREATIVE Inawaletea picha za tukio la Harusi ya nguvu iliyofanyika Jumamosi Tarehe 25 septemba 2011 Katika ofisi ya Reading Registrar kati ya Katibu wa Tawi la TA Hapa Mjini Reading Amri Dello na Alice Kapya.
Baada ya Kufunga pingu za maisha tafrija ilifanyika ndani ya Boat na kuzunguka mitaa ya berkshire hadi windsor kwa Queen na kumalizikia katika Mji wa Reading.
Wadau mbalimbali walikuwepo katika sherehe hii akiwepo Mh Balozi wetu Peter Kallaghe.
URBAN PULSE inapenda kuwapa hongera sana Maharusi wetu na kuwatakia kila la kheri katika safari yao ndefu walioianza leo.
MUNGU AWABARIKI,
Asanteni
URBAN PULSE CREATIVE
Comments
Post a Comment