Mh. Naibu Balozi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe walioteuliwa kuwakilisha katika Bunge la vijana Lucy Minde (kushoto) na Linda Kapinga (kulia)
Linda Kapinga mteuliwa mmoja wapo
Lucy Minde mteuliwa wa pili
Lucy akitoa ufafanuzi wakati wa mahojiano
Urban Pulse na Miss Jestina wakifanya mahojiano na Linda
Kushoto Lucy na Lindi wakiwa katika picha ya pamoja ubalozini
Mh. Naibu Blozi kwenye picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa ubalozi, TMK na mapromota wao, walikuja kuwaunga mkona Linda na Lucy
Salam,
Ubalozi wetu wa Tanzania Hapa Nchini Uingereza Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wamewateua Linda Kapinga na Lucy Minde ili kwenda kutuwakilisha katika mkutano wa nne wa Commonwealth Youth Parliament ( Bunge la Vijana) ulioanza tarehe 6-10 Septemba 2011 jijini London. Mkutano huu Umeandaliwa na Commonwealth Parliamentary Association tawi la Uingereza ikishirikishwa na Sekretarieti ya CPA ambayo ni Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Katibu wake ni Mwafrika wa kwanza kuteuliwa na Pia ni Mtanzania mwenzetu Dr William Shija.
Lengo kuu la mkutano huu ni kuwawezesha vijana kati ya miaka 19-29 kwa kuwapatia uzoefu wa shughuli za Bunge hasa katika kuimarisha demokrasia ya mabunge na Uchumi. Motto wa Mkutano wa mwaka huu "MABADILIKO YA HALI YA HEWA"
Ubalozi wa Tanzania hapa Uingereza unapenda kuwapongeza sana Linda Kapinga na Lucy Minde kwa kuchaguliwa kwao na pia kuwatakia kila la kheri katika kutuwakilisha kwenye mkutano huu.
Asanteni,
Urban Pulse ikishirikiana Miss Jestina Blog Na Ubalozi wa Tanzania
Comments
Post a Comment