TUSOME VITABU ni kipindi kipya cha redio kitakacho kujia hivi karibuni kupitia kituo chako cha redio ukipendacho '" PASSION FM " cha jijini Dar es salaam. Madhumuni ya kipindi ni kuwaelimisha na kuwahamasisha watanzania umuhimu wa kusoma vitabu. Na Malengo ya kipindi hiki ni kutengeneza jamii ya watanzania wenye kupenda na kuthamini kusoma vitabu . Tutakuwa tukifanya mahojiano na waandishi pamoja na watunzi mbalimbali wa vitabu bila kusahau kuvifanyia uchambuzi wa kina vitabu hivyo. Kama wewe ni mwandishi ama mtunzi wa vitabu na ungependa kushiriki katika kipindi hiki tafadhali wasiliana na waandaaji wa kipindi kwa simu namba : 0767010756. Tunakaribisha watunzi wa vitabu vya aina zote, yaani vitabu vya ziada na kiada, vitabu vya kitaaluma na vitabu viusivyokuwa vya kitaaluma.Ewe mwandishi , ewe mtunzi wa vitabu, tumia nafasi hii ya pekee kutangaza kitabu chako. Usibakie kusema tu " Watanzania ni wavivu wa kusoma vitabu wakati hujakitangaza kitabu chako "KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA : 0767010756
Comments
Post a Comment