WAUMINI WA DINI YA SIKH SOUTH HALL UK WASHEREKEASIKU YA KUZALIWA MWANZILISHI WA DINI HIYO GURU NANAK...!!!
Muasisi wa dini ya Sikh Guru Nanak
Maandamano yakiendelea
Waumini wa dini ya Siki wakihidinisha siku yao
South Hall palikuwa hapatoshi
Wakati wa kupata mapocho pocho
Hata watoto walikuwepo wakisaidia kutayarisha chakula
Frank akiwa katikati y amitaa ya Southall kushuhudia sherehe hii
Frank akipata chai ya tangawizi na hiliki kutoka India
Wadau wakiwa kazini wakitayarisha chakula
**************
Salam,
Maelfu ya wafuasi wa dini ya Sikh walijitokeza siku ya Jumapili tarehe 6 Novemba 2011 katika mjini wa Southall, Middlesex UK ili kusherekea siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa dini yao Guru Nanak aliezaliwa mwaka 1469 nchini Pakistani.
Wakati akiwa na umri wa miaka 30 alipotea kwa hali ya miujiza kwa mda wa siku tatu. Alipo rejea alianza kuhubiri, kufundisha na kuandika dini ya Sikh wakati maisha yake yote. Pia Guru Nanak alisafiri dunia nzima kuitangaza na kujadili dini hii kwa waumini wengine kama waislamu pamoja na Hindus
Kwa Miaka zaidi 550 wafuasi wa dini hii wamekua na desturi hii ya kusherekea siku moja kabla ya kuzaliwa kwake Guru Nanak kwa kuandaa maandamano haya makubwa ya Sherehe hii ambayo hufanyika India pamoja na baadhi ya sehemu za nchi ya Uingereza. Kwa kawaida sherehe hizi huongozwa na wafuasi wakuu watano wanaojulikana kama ''Panj Piare'' wakiambatana waimbaji, wanamuziki na timu ya wacheza upanga (Martial Arts) kuelekea hekaluni kwao ''Gurdwara'' Sri Guru Singh Sabha, hapa Southall hekalu lao ndio kubwa kuliko yote katika bara la ulaya
Sherehe hizi huanza mapema asubuhi kwa kuimba, kuomba kwa pamoja. Baadae chakula cha kitamaduni kinachojulikana kama ''Langar'' hutolewa bure kwa kila mtu.
Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE
Comments
Post a Comment