MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa
Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu
katika pambano lisilo la ubingwa. Pambano hilo linatarajia kuwa la
raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni
Kijichi jijini Dar es Salaam .
Siku kumi kabla ya mpambano mabondia Rashidi Matumla na Maneno
Osward walishauliana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa
ya kuongeza nguvu kama wanatumia na wameshapimwa na Daktali wa mchezo
wa ngumi nchini chales kilaga, sheria za mchezo huo azirusu kutumia dawa
za aina yoyote ya kuongeza nguvu. Hivyo mabondia wote wamekutwa wapo fiti na wanatarajia kuzipiga jumapili ya tarehe 25
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios 'mwayamwaya' ambaye ndiye
muandaaji wa pambano hilo, alisema pambano hilo limeandaaliwa ili
kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho
Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa
hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo
Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja
mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.
Utasindikizwa na mabondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa
Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga
atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi
pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na
kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya
kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za
masumbwi.
Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.
'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,
DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

Comments
Post a Comment