RAISI JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WATU KATIKA MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA MAREHEMU REGIA MTEMA IFAKARA MOROGORO...!!!

Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye mazishi ya Marehemu Regia Mtema na kuongoza mamia ya waombolezaji wa mji wa Ifakara kwenye mazishi hayo jana ambapo pia viongozi mbali mbali walishiriki.Wengine pichani ni Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda (pili kulia),Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai (kulia),Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe, na kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe.
 Rais Kikwete akiongea na Spika Anne Makinda. Pembeni yao ni Naibu Spika Job Ndugai na Mh Hawa Ghasia
 Viongozi wa CHADEMA msibani
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya Marehemu Regia Mtema mjini Ifakara
 Vijana wa ulinzi wa CHADEMA wakithibiti umati wa waombolezaji
  Baadhi ya wabunge toka vyama mbalimbali wakiwa mazishini 
  Umati wa waombolezaji makaburini 
  Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe alipowasili
  Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa makaburini
  Mwili wa marehemu ukiwasili makaburini
 Mdogo wa marehemu 
  Wanahabari wakirekodi tukio hilo
  Vilio na majonzi
 Pacha wa marehemu akibembelezwa
  Sehemu ya waombolezaji
 Kwaya ikiimba mapambio  
  Wazazi wa marehemu
  Ibada ya mazishi ikiendelea

 Salamu za Shukrani toka kwa msemaji wa familia 
 Wazazi wa Marehemu wakiweka udongo kaburini
 Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Regia Mtema aliezikwa leo Ifakara Mkoani Morogoro.
  Spika Anne Makinda akiweka udongo kaburini
  Naibu Spika akiweka udongo kaburini
  Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akiweka udongo kaburini
 Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kuweka shada la Maua kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Regia Mtema aliyoongoza mjini Ifakara mkoani Morogoro leo.
 Rais Jakaya Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Regia Mtema ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Jimbo la Morogoro aliefariki kwa ajali ya gari maeneo ya Ruvu mkoani Pwani hivi karibuni .  
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa akijiandaa kuweka shada ya maua kaburini
R.I.P Regia Mtema
Picha kwa hisani ya Michuzi

Comments