Kaimu MKurugenzi Ukaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Pesheni wa Utumishi wa Umma PSPF. Bw. Godfrey Ngonyani (kushoto) akikabidhi msaada wa Madawati 60 yenye thamani ya milioni tatu walioutoa leo kwa Mjumbe wa Kamati ya Shule Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani, Bi. Jacklin Kitego kulia na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Anifa Kombo.
Kaimu MKurugenzi Ukaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Pesheni wa Utumishi wa Umma PSPF. Bw. Godfrey Ngonyani (kulia) akizungumza na Wazazi na Wanafunzi pamoja na Bodi ya Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani wakati walipokwenda kukabidhi msaada wa Madawati 60 yenye thamani ya milioni tatu kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Bi. Anifa Kombo na Mjumbe wa Bodi ya PSPF Bw. Ramadhani Maneno.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani wakigombania kukaa kwenye madawati mapya walioletewa na Mfuko wa Pesheni wa Utumishi wa Umma PSPF.
(Picha na Rajabu Mhamila 'Super D')
Lini watatoa maeneo mbali yasiyo kuwa nyumbani kwa Rais au wabunge? Its sad utasikia wanapewa shule za mjini tu zile za pembezoni husikii... Nadhani watumishi walio staafu wako Mbambabay, Longido, Kantalamba, Ikuti etc...
ReplyDelete