Marehemu Christavina Cryor Kusaga
---
Familia ya Kusaga na Mume wa Christavina, Lavorn Cryor wanasikitika kutangza Kifo cha mpendwa wao Christavina Cryor kilichotokea Feb, 7 Nyumbani kwake kwa Saratani ya Utumbo (Colon Cancer).
Christavina alianza kuugua tangia August 2011 na kulazwa Holy Cross Hospital na baadae kuhamishiwa Georgetown University Hospital.
Na aliruhusiwa juzi Feb 6, 2012 saa 3 usiku arudi nyumbani ni kama alikuja kumuaga mume wake na watoto ndipo ilipofika saa 8 usiku wa kuamkia jana Feb 7, 2012 akafariki.
Marehemu alizaliwa October 12, 1983, ameacha Mume na Watoto wawili, wakiume miaka 4 na wa kike miaka 2.
Katia husia, marehemu aliomba azikwe hapa kusudi awe karibu na wanae na mume wake.
Kwa wale ambao hawataweza kufika msibani lakini watapenda kutoa rambirambi kwa mchango wa fedha, tafadhali tumia huduma ya benki kama ifuatavyo.
Capital One Bank, NA
Routing Number: 255071981
Account Number: 1351500235
Tunatanguliza shukrani zetu kwa msaada katika kufanikisha shughuli za msiba huu
Msiba upo: 3237 75th Avenue Apt 201,
Landover, MD 20785.
Taarifa nyingine mtaarifiwa baadae tunaomba tujumuike pamoja tuweze kuwafariji wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.
Comments
Post a Comment