WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUKUTANA NA MADKTARI UKUMBI WA CPL HOSPITALI YA MUHIMBILI KESHO, TAREHE 9 FEB 2012 SAA 3 ASUBUHI...!!!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
---
Waziri mkuu Mhe. Mizengo Pindo yupo Dar Es Salaama kutoka Dodoam kushugulikia mgomo wa Madaktari ambao umekuwa ukiendelea kwa kwa lengo la kuupatia ufumbuzi.


Waziri Mkuu amekutana na uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na madaktari bingwa kutoka sekta ya UMMA, Binafsi na Wastaafu. 


Mhe. Pinda atakutana na madaktari Bingwa, madakatari waliosajiliwa (Registrals) na madaktari walioko kwenye mafunzo kwa vitendo (Interns) hao kesho tarehe 9 Feb 2012 saa 3 asubuhi na baada ya hapo saa 4 atakutana na wafanyakazi wa hospitali ya Muhimbili, MOI, Ocean Road na wawakilishi kutoka Hospitali za Mkoa wa Dar Es Salaam, kwenye ukumbi wa CPL, Muhimbili.


Matarajio ya Serekali ni kwamba mazungumzo hayo yataweza kumaliza mgogoro huu na madaktari wote kurejea kazini na hivyo kurejesha huduma za matibabu katika hali ya kwawida kwa wananchi wa Tanzania.


Hivyo Serekali inawaomba wahusika wote wafike katika mikutano hiyo bila kukosa

Imetolewa na ofisi ya Waziri Mkuu

Comments