Wengi wetu hupenda kuiga ‘mitindo ya ng’ambo’ Kama waiitavyo wanaoipenda, na wasioipenda mitindo yenyewe.
Ni muhimu kujua kuwa mengine huwa na madhara zaidi hata kuliko burudani…hasa mtindo huu wa kujichora mwilini.
Mapenzi kwa SANAA hasa ya kuchora huwafanya watu kupata michoro midogo modogo kama vile maua, vikaragosi na kadhalika…lakini WENGINE WAMEZIDI!!!
Ni vyema kukumbuka kuwa kuna hatari nyingi katika jambo kama hili na kuongea kuzihusu itakuwa kama kuimba nyimbo ambayo husikilizwa kila asubuhi redioni.
TRAVIS BARKER ameamua kuongeza michoro hii hadi kichwani.Yeye siye wa kwanza kufanya hivi..ndio ..lakini jambo hili bila shaka LITAIGWA NA WATU KADHAA WANAOISHI KWA MSEMO,.. “NAMPENDA NA ANAFANYA, MIMI PIA NITAFANYA”
Tuzinduke, tuamke!!
Comments
Post a Comment