THE MILLEN MAGESE MODEL SEARCH 2012 MAMIA WAJITOKEZA...!!!

 Majaji Mustafa Hassanali, Madame Rita Paulsen (kulia), Aminat  Ayinde na Doreen Noni (shoto) wakipozi kabla ya kuanza zoezi hilo leo hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Millen Magese akiwakaribisha mamodo watarajiwa
 Aminat  Ayinde kutoka America  Next top model cycle 12 ya Tyra  akisaidia katika zoezi hilo
Mamodo watarajiwa wakisubiri kusailiwa
Mamodo watarajiwa wakiwa wanasikiliza kwa makini
Mamodo
Palijaa sana
Mamodo zaidi
Full house
Mrembo kutoka Miss Tanzania 2nd runner up 2011 Alexia William nae alikuwepo
Mamodo wakifuatilia issue kwa umakini
---
Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese leo ameendesha zoezi la kutafuta wanamitindo watano (wa kike watatu na wa kiume wawili) watakoshiriki kwa mara ya kwanza katika  maonyesho  ya wiki ya Mavazi ya Afrika Kusini (South Africa Fashion Week) tarehe 1 April mwaka huu.Mamia ya wasichana na wavulana wamejitokeza katika zoezi hilo hoteli ya Serena ambalo Millen ameliandaa kupitia kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Millen Magese Group Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo (Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX).Millen  anaamini kuwa wanamitindo wa Tanzania watakaopatikana katika zoezi hilo wataiwakilisha Tanzania vyema katika wiki ya maonyesho ya mavazi ya Afrika Kusini na kuitangaza Tanzania kimataifa kama anavyofanya yeye kwa hivi sasa.Wanamitindo waliotakiwa walitakiwa kuwa  na vigezo vifuatavyo vya:- Umri miaka 18 mpaka 24, urefu 1. 75m, hips 37cm (ukiwa na nywele zako za asili) na kwa wanaume urefu ni 1.82m.“Naamini kuwa zoezi hili litawanufaisha wana mitindo wa kike na wa kiume wa Tanzania na vile vile ushiriki wao katika SAFW na katika maonyesho mengine ya mavazi nje ya Afrika na kusaidia kuitangaza nchi kimataifa,” alisema Millen.Alisema kuwa lengo kubwa la kampuni yake ni kuendeleza fani ya uanamitindo na vile vile kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake kwa kupitia fani ya mitindo na hata kwa njia ya utalii.Aliongeza kuwa japo Tanzania ina wanamitindo wengi na wabunifu, bado kuna pengo kubwa ukilinganisha na maendeleo ya fani hiyo katika nchi ya Afrika Kusini na Nigeria.Alisema kuwa nchi hizo zimepiga hatua kubwa sana na yeye kuhamasika kuanzisha kampuni yake iliyozinduliwa mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuziba pengo hilo na kuleta maendeleo ili wahusika wafaidike na matunda ya fani yao.Majaji wa zoezi hilo ni Ritha Poulsen, Mustapha Hassanali na Khadija Mwanamboka na katika kuwekea umuhimu zaidi mchakato huo, MMG imemkaribisha mwanamitindo maarufu, Aminat  Ayinde kutoka America  Next top model cycle 12 kushuhudia zoezi hilo lililodhaminiwa na Clouds FM na Benchmark production.
Picha kwa hisani ya Michuzi

Comments