VIDEO NA PICHA: WASANII WA MNANDA, MDUARA, AKINA RIHANNA, EXTRA BONGO NA IZO BUSINESS WATIKISA NDANI YA DAR LIVE...!!!
Msanii AT akiwarusha wapenzi wa mduara.
Wasanii wa kundi la Offside Trick wakilishambulia jukwaa.
Dogo Mfaume akizikonga nyoyo za mashabiki wa mnanda.
Msanii Easy Man akikamua stejini.
Msanii Hammer Q akikoleza burudani hizo.
AT na Shilole wakiwapagawisha mashabiki.
Bendi ya Extra Bongo ikiongozwa na Ali Choki kutoa raha kwa mashabiki.
Msanii aliyepanda stejini kama 'suprise' Izo Business akiwasabahi mashabiki kwa songi lake la Ridhiwan.
Mnenguaji wa kundi la Shilole akionyesha ujuzi.
Washiriki wa shindano la Vaa, Imba na Cheza kama Rihanna walioingia sita bora wakiwa katika pozi.
Nyomi iliyoitikia shangwe hizo.
---
WASANII Dogo Mfaume, Easy Man na kundi la Jaguar jana walifunika vilivyo kwa upande wa Mnanda huku Offside Trick wakisindikizwa na Hammer Q, AT na Shilole wakiangusha bonge la burudani na kuwarusha vilivyo wapenzi wa Mduara waliofurika katika ukumbi wa maraha wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem. Bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo nayo haikuwa nyuma kukonga nyoyo za mashabiki wakati washiriki wa shindano la Vaa, Imba na Cheza kama Rihanna wakitikisa na kuwaacha midomo wazi wapenzi wa shangwe mahali hapo. Msanii Izo Business aliyepanda stejini kama ‘surprise’ naye alifanya kweli kwa kuwarusha mashabiki na songi lake kali la Ridhiwan.
Cheki makamuzi yalivyo kuwa:
Mkali wa Mnanda, Easy Man akiwapagawisha wapenzi wa burudani waliofurika katika Ukumbi wa Kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem Jumapili, Machi 11, 2012 wakati wa Tamasha la Mduara Vs Mnanda.
Msanii Dogo Jack kutoka Kundi la Mnanda la Jaguar akifanya makamuzi katika Ukumbi wa Dar Live Jumapili Machi 11, 2012.
Comments
Post a Comment