Video clip 1
Video clip 2
MAMBO BADO HAYAELEWEKI KATI YA SEREKALI NA MADAKTARI
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
---
Ule mgomo wa madaktari uliotangazwa kufanyika leo umeanza katika mazingira ya kimyakimya. Hii imebainika pale mwandishi wetu alipotembelea hospitali hiyo ili kujionea kile kichokuwa kimekusudiwa.
Hali ilivyokuwa katika hospitali hiyo kuu ya taifa kwa siku ya leo ni kwamba hakuna daktari hata mmoja aliyekuwa anashughulika na mgonjwa bali manesi tu ndiyo waliokuwa wanashughulika na wagonjwa wa zamani na si wapya ambapo.
Uchunguzi uliofanywa hospitalini hapo ni kuwa kila idara ilikuwa na mikutano katika kujadili hotuba ya waziri mkuu aliyoitoa jana ikiwa inalenga kuwasihi madaktari waache mgomo bali waendelee kufanya kazi huku suala lao likiwa linashughulikiwa.
Kwa upande wa madakari hao wameazimia kwa pamoja kuwa mgomo huo unaanza rasmi leo baada ya kikao hicho na kuwataka wananchi wawaelewe kuwa lengo lao ni kuboresha maslahi yao.
Kwa mara nyingine Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema kama wanakusudia kufanya mgomo huo basi serikali imejiandaa kwa kila hali ili kukabiliana na mgomo huo.
Katika mazingira ambayo yanaweza kuitwa tata siku ya kesho haileweki hali itakuwaje kitu ambacho wagonjwa wengi wamepewa tarehe za mbele hali ambayo wengi wao imesononeshwa na ahadi hizo.
Mwandishi wetu alipojaribu kumtafuta msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Ameniel Aligalesha, aliambiwa kuwa yupo katika kikao ndani ya hospitali hiyo na lengo lilikuwa ni kujadili na kufikia maamuzi ya hotuba ya waziri mkuu.
Hadi leo Pinda ameishakaa mikutano mbalimbali kujadili swala hilo la madaktari. Kwa mara ya kwanza ilikuwa Januari 29 mwaka huu katika ukumbi wa Karemjee aliposema kuwa daktari ambaye angegome angejifukuzisha kazi na akapiga marufuku mikutano yao kufanyika kokote.
Februari 9 alikutana na madakari bingwa na watumishi wa hospitali za Temeke, Ilala, Mwananyamala na Muhimbili.
Na jana alikutana na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo aliyakataa masharti ya madaktari ambayo waliyatoa ili waweze kuendelea na mazungumzo na serikali.
Baada ya madaktari kukaa leo, Pinda amesema kama wametangaza mgomo serikali iko tayari kukabiliana na mgomo huo.

Video kwa hisani ya kennedytz.blogspot.com
Comments
Post a Comment