Habari za muda huu zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi limeanza kumhoji 'mtoto' anayeshukiwa kuwa chanzo cha Steven Kanumba (The Great), Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la kisanii, Lulu, amekanusha kumsukuma msanii huyo nguli hadi kufa.
Amesema kamwe hakufanya hivyo, pamoja na kwamba walikuwa wamekwaruzana kwa muda mfupi na akaenda kuoga, akiwa anatoka bafuni alianguka (aliteleza) na kugonga kichwa kabla ya kukutwa na umauti.
Binti huyo ameiambia Polisi kwamba Kanumba (ambaye wamekuwa na uhusiano naye wa mapenzi kwa muda sasa) alikuwa 'amebugia' ujazo mkubwa wa pombe kali aina ya Jack Daniels (JD). Uchunguzi bado unaendela.
Blog hii itaendelea kukutaarifu juu ya juu ya mkasa huu unaoonekana kuvuta hisia za Watanzania wengi na hata wale walio nje ya nchi.
Habari hii ni kwa hisani ya Tanzania Journalists Alliance (TAJOA)
Jamani huyu kanumba (rip) si alikuwaga anasema hanywi pombe? nimechanganyikiwa!!! ntarudi badae
ReplyDeleteSasa unaona yeye mwenye ndio kanguka kwa bahati mbaya.alifikirije mbombe sio tea tena pombe yenye kali ni lazima itakuwa pombe ndio iliyo mmaliza masikini kaka kaka watu hakujua pia yeye mwenye alisema kwa salama kwa hanyu pombe labda alikuwakutoa ushai mbele ya binti mhhh hii kali
ReplyDeletedah we wl 4evr mc hm
ReplyDeletesasa alikuwa anaongea na nani..si ataje na yeye.
ReplyDeleteHalafu dada mtu anayesema kaka alisukumwa ma walikuwa wamejifungia ndani alionaje!!!
Hilo neno.....simply because walikuwa wawili ndani ndo tuseme KASUKUMWA?!....hAIINGII AKILINI
ReplyDelete