Abiria 35 na wafanyakazi wane wa ndege ya shirika la Ndege Tanzania (ATC) wamenusurika katika ajali ya ndege (pichani juu) iliyotokea asubuhi ya leo majira ya saa 4.15 katika uwanja wa ndege wa Kigoma.
Habari za awali zinasema, ndege hiyo aina ya Dash 8-300 iliyokuwa inatoka Kigoma kwenda Dar es salaam kupitia Tabora ilipata ajali baada ya kuteleza nan kuangukia ubavu wa kulia kutokana na tope jingi lililokuwepo katika njia ya kurukia ya uwanja huo.
Abiria na wafanyakazi wote waliokuwamo waliweza kutoka katika ndege salama muda mchache baada ya jaribio lake la kupaa angani liliposhindikana.
Baadhi ya abiria waliohojiwa baada ya ajali wamewasifia sana rubani Emmanuel Mshana na msaidizi wake Mbwali Masesa kwa kujitahidi kuidhibiti kiuweledi ndege hiyo na kuokoa maisha ya watu.
Uchunguzi wa awali unaonesha bawa la kulia pamoja na injini ya propela ya upande huo vimeharibika vibaya.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma SSP Kihenya akiwa eneo la tukio.
Picha na Mbwate wa Jeshi la Polisi
Uwanja wa ndege ulijaa tope? Haha!
ReplyDeleteJamani jamani acheni dharau mnahatarisha maisha ya wananchi
ReplyDelete