WASANII WEMA SEPETU NA IRENE UWOYA NI MIONGONI YA WATU 200 WALIO ZIMIA KWENYE MAZISHI YA KANUMBA...!!!
Wema Sepetu akimbizwa hospitali... Baada ya kuzidiwa na kuanguka!! Makaburini kabla mwili wa marehemu kufika.
---
ZAIDI ya watu 200 waliishiwa nguvu na kuanguka wakati wa mazishi muigizaji maarufu Steven Kanumba, miongoni mwao wakiwamo wasanii wawili maarufu nchini, Irene Uwoya na Wema Sepetu.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Slaam leo, Mwenyekiti wa Tiba na Kamati ya Mzishi Dk. Nassoro Ally alisema kuanguka kwa watu hao kumetokana na mkusanyiko mkubwa wa watu ambao ameulinganisha na ule ulijitokeza wakati wa mazishi ya Julius Nyerere.
Alisema hata hivyo, baadhi ya watu hao walioanguka wengi wao walipatiwa huduma ya kwanza akiwamo Uwoya na watu wa Msalaba Mwekundu na kisha kuruhusiwa kuendelea na shughuli za mazishi za muigizaji huyo maarufu Barani Afrika.

Irene Uwoya akipewa hudum ay akwanza baada ya kuzimia
---
Dk. Ally alisema hali hiyo,imekuwa ikijitokeza katika mikusanyiko ya namna ile ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa ya moyo, kukosa hewa ya kutosha na wengine kuanguka kutoka juu ya miti walikokuwa wamepanda kushuhudia tukio hilo.
Kwa upande wa muigizaji Wema Sepetu hali ilikuwa mbaya ukilinganisha na mwenzake Uwoya kwani ilibidi akimbizwe katika hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.
Kwa upande wa muigizaji Wema Sepetu hali ilikuwa mbaya ukilinganisha na mwenzake Uwoya kwani ilibidi akimbizwe katika hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.
Baada ya kupata haafueni,Wema Sepetu aliongea na Ripota Wetu aliefika hospitalini hapi na akiwa kitandani alisema alijisikia ghafla akiishiwa nguvu na kushindwa kujitambua na kujikuta akianguka na kupoteza fahamu.
Alisema hali hiyo imechangiwa na njaa kwani alifika katika maeneo viwanja vya Leaders akiwa hajapata hata kifungua kinywa, joto kali huku akizunguukwa na watu wengi kila alipokuwa akikaa.
Alisema hali hiyo imechangiwa na njaa kwani alifika katika maeneo viwanja vya Leaders akiwa hajapata hata kifungua kinywa, joto kali huku akizunguukwa na watu wengi kila alipokuwa akikaa.
Baadhi ya waombolezaji waliozimia msibani hapo wakipewa hudum aya kwanza
---
Awali msemaji wa Hospitali hiyo ya Mwananyamala Edward Bisekala alisema hali yake siyo mbaya kama mnavyomuona akiwa na drip ambapo hali hiyo imesababishwa pressure.
Hadi Ripota huyu anaondoka hospitalini hapo kulikuwa na watu wapatao wanne wakiwa wamewekewa drip ambapo pia hali zao hazikuwa mbaya.
Aidha, katika hatua nyingine baba mzazi wa muigizaji huyo, Mzee Charles Kanumba alisema malengo ya mwanaye kisiasa ilikuwa agombee ubunge mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kwa mujibu wa Redio Wapo Kanumba alimwambia baba yake nia yake hiyo ambapo alikubaliwa na kuambiwa kuwa hilo ni chaguo lake kwani ana haki ya kuamua anachokipenda.
Kwa mujibu wa Redio Wapo Kanumba alimwambia baba yake nia yake hiyo ambapo alikubaliwa na kuambiwa kuwa hilo ni chaguo lake kwani ana haki ya kuamua anachokipenda.
Mzee Kanumba alisema mipango yake hiyo ilikuwa ikienda vizuri kwani wakazi baadhi ya vijana walikuwa wakimuunga mkono kutokana na nia yake hiyo.
Source: Michuzi
Comments
Post a Comment