BALOZI PETER KALLAGHE AWASILISHA BARUA YAKE YA UTAMBULISHO IRELAND...!!!

 Mh. Balozi Peter Kallaghe akiwasilisha barua ya utambulisho kwa Rais wa Ireland Michael Higgins
 Mh. Balozi Peter Kallaghe katika picha ya pamoja  na Rais wa Ireland Michael Higgins mara baada ya kuwasilisha barua ya utambulisho
 Mh. Balozi Peter Kallaghe na mke wake Mama Balozi Joyce Kallaghe katika picha ya pamoja  na Rais wa Ireland Michael Higgins mara baada ya kuwasilisha barua ya utambulisho
Afisa ubalozi Amos Msanjila na Mh. Balozi Peter Kallaghe katika picha ya pamoja na Rais wa Ireland Michael Higgins mara baada ya kuwasilisha barua ya utambulisho.
---
"Mheshimiwa Balozi Peter A. Kallaghe jana amewasilisha rasmi barua yake ya utambulisho (Letter of Credence) kwa Mheshimiwa Rais wa Ireland Michael Higgins katika sherehe fupi iliyofanyika katika Ikulu ya nchini hiyo jijini Dublin. Pamoja na barua hiyo Balozi Kallaghe aliwasilisha rasmi salamu za Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikimtakia Rais Higgins  afya njema na furaha. Nae Rais Higgins alipokea salamu hizo kwa kusifu uhusiano wa kihistoria kati ya nchi hizi mbili. Alimkumbuka Baba wa Taifa, Marehemu Mwalimu  Julius Nyerere kama mtu  shupavu aliyeijengea Tanzania misingi thabiti ya  kisiasa na kiuongozi. Aidha alikumbuka uzuri wa Tanzania na wananchi wake, alioushuhudia alipotembelea Kilosa, mkoani Morogoro miaka ya  1980. Katika shughuli hiyo Balozi Kallaghe alisindikizwa na Mkewe Joyce na Afiisa wa Ubalozi Amos Msanjila. Pamoja na kuiwakilisha  Tanzania, Uingereza, (United Kingdom) Ubalozi wa Tanzania London unaiwakilisha nchi pia huko Ireland. Tanzania ni moja ya nchi saba tu zinazopata misaada ya kimaendeleo toka Ireland, hasa kupitia taasisi yao ya Irish Aid.  Nchi zingine ni Ethiopia, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Uganda na Zambia."

Comments