Pichani (kushoto) ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Mh Benjamini Mkapa akichangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika, mapema jana jioni, mkutano huo umefanyika kwenye moja ya kumbi ya chuo kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini. Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na mwisho ni Rais mstaafu wa Benin, Nicéphore Dieudonné Soglo.
Pichani kulia ni Rais mstaafu wa Benin, Nicéphore Dieudonné Soglo akifafanua jambo kwa makini wakati wa mchakato wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ulipokuwa umepamba moto jana jioni, katika mkutano uliofanyika kwenye moja ya kumbi ya chuo kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini, Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Mh Benjamini Mkapa.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano huo.
Pichani juu na chini Mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ukiendelea ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini jana mchana.
Baadhi ya Marais Wastaafu kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania, ambaye pia ni Mratibu mkuu wa mkutano akifafanua jambo kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Mkutano huo mapema jana mchana.
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakijadiliana jambo nje ya ukumbi, kabla ya kuanza kwa Mkutano huo, Shoto ni Absolom Kibanda (Free Media), Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications), Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper) na Muondosha Mfanga (The Guardian).
Baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja jana kabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika, ambao umewashirikisha Marais Wastaafu nane wa Afrika.
---Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wakutana nchini Afrika Kusini
Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wamekutana jana jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kufanya mkutano wa siku tatu ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand. Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
---Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wakutana nchini Afrika Kusini
Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wamekutana jana jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kufanya mkutano wa siku tatu ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand. Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
Marais wastaafu hao waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania, Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin, Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania, Rais Joaquim Chissano wa Msumbiji, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Rais Rupiah Banda wa Zambia.
Aidha - mbali ya Marais hao waliohudhuria mkutano huo, pia ulihudhuriwa na Wataalam mbalimbali wa nishati, viongozi wa umma na sekta binafsi na wanafunzi na kitivo kutoka vyuo vikuu 9 vya kimataifa kikiwemo chuo kikuuu mwenyeji cha Witwatersrand a.k.a Wits. Tanzania iliwakilishwa na wanafunzi watano na walimu wawili kutoka chuo kikuu cha Dar-es-Salaam.
Mratibu mkuu wa mkutano huo - Balozi Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadiliana juu ya ufumbuzi wa mageuzi ya nishati katika nchi za Kiafrika, na kuhakikisha nchi za Afrika zinajiwakilisha vyema katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala zima la Nishati. Balozi Stith alisema kuwa mkutano huo utaleta mshikamano wa pamoja kwa viongozi wa sekta ya nishati na wafadhili mbalimbali wa miradi mbalimbali, ili kuhakikisha nishati hiyo inatosheleza mahitaji ya Afrika kwa ujumla. Mkutano huo wa siku 3 utafikia tamati Mei 25.
Comments
Post a Comment