Msanii Steven Mangele katikati akiwa na Ofisa wa Kampuni ya Steps Pritesh Chavda na Mwandishi wa habari wa kituo cha EATV wakati alipokwenda kutembelea kituo cha watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni na kutoa Zawadi ya vyakula mbalimbali kwa ajili ya uzinduzi wake wa filamu ya 'Nyerere' leo
Steven Mengele 'Steve Nyerere' kushoto akimkabidhi chandarua mtoto Ali Husein wakati alipokwenda kutoa misaada mbalimbali na kufanya utambulisho wa filamu yake mpya ya Nyerere
Steven Mengele 'Steve Nyerere' kushoto akimkabizi maharage kwa mama mrezi wa kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Dar es salaam Bi. Zainabu Bakari alipokwenda kutoa misaada ya vyakula na vitu mbalimbali leo
Steven Mengele 'Steve Nyerere' katikati akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Maunga Kinondoni Dar es salaam leo
Steven Mengele 'Steve Nyerer' akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kwa ajili ya kutambulisha filamu yake ya Nyerere
Msemaji wa Kampuni ya Steps ya jijini Dar es salaam Kambarage Ignatios akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa filamu ya Mwalimu Nyerere leo
Mkurugenzi wa DJ. Marketing and Promotion, Daniel Haule kushoto na Msemaji wa Kampuni ya Steps ya jijini Dar es salaam Kambarage Ignatios ambao hufanya kazi za kubandika mabango mbalimbali kwa usafi wa hali ya juu kwa ajili ya kutoalibu mazingira akibandaka bango la filamu mpya ya Nyerere iliyozinduliwa leo
---
MSANII wa filamu nchini ambaye pia huiga sauti za viongozi mbalimbali, Steve Mengele 'Steve Nyerere' jana amezindua filam yake mpya inayojulikana kama 'Mwalim Nyerere'.
Filam hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua Ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filam hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 3 ikiwa ni pamoja na kujitolea kuwasomesha watoto wawili katika kituo hicho.
Akizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Steve Nyerere alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba Baba wa Taifa Mwali Nyerere hakubagua watu.
Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha anamuenzi Baba wa Taifa kwa kutoa filamu itakayokuwa inaonesha mambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya Baba wa Taifa.
"Jina lililonibeba zaidi katika tasnia hii ya filamu ni jina la Steve Nyerere kiasi ambacho hata jina la Baba yangu halijanizoea, hivyo kutokana na ukubwa wa jina hili limenifanya mimi kutambulika na jamii nzima ya Tanzania hivyo ili kulienzi jina hili nimeamua kutoa filamu hii ya Mwalim Nyerere,"alisema Steve.
Alisema msaada alioutoa kwa watoto yatima hautaishia kwao bali ataendelea kutoa kile atakachokipata kupitia filamu hiyo kuwasaidia na wale wasiojiweza.
Alisema filam ya Mwalim Nyerere ameifanyia Butiama alipozaliwa Baba wa Taifa ili kujenga uhalisia wa kile alichodhamiria na kwamba ameitengeneza filamu hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu huku akishirikiana vema na mke wa Hayati Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.
Alisema jumla ya sh. milioni 25 ametumia katika kuikamilisha filam hiyo ambayo itaanza kuingia sokoni leo ikiwa chini ya usambazaji wa Steps Entertaiment.
Kabla ya kutoa filam hiyo Steve Nyerere alitamba na filam ya 'Mr President' aliyoitunga kwa kuvaa uhusika wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete ambayo aliitaja kama zawadi kwa Rais Kikwete katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika

Comments
Post a Comment