Sugu akiwarusha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Sugu na Mkoloni wakizidi kuwadatisha mashabiki.
Cheki video ya makamuzi ya Mh. Sugu ndani ya Dar Live
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari nae akitoa 'verse' kuupamba usiku wa Sugu ndani ya Dar Live.
Profesa Jay akiwapa burudani mashabiki wa Dar Live.
..Akiwasabahi mashabiki wake.
Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi likifanya makamuzi stejini.
....Wanaume kazini.
Mapacha kutoka kundi la Vinega wakiiteka steji ya Dar Live.
Suma G nae alikuwepo kuupamba usiku huo.
Danny Msimamo akiwarusha wapenzi wa burudani.
Bendi ya Chuchu Sound nayo ilifanya makamuzi katika tamasha hilo la Usiku wa Sugu.
Kundi la Naukala Ndima likifanya vitu vyake stejini.
Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan akiwasalimia mashabiki wa Dar Live.
Nyomi iliyohudhuria Usiku wa Sugu.
Baadhi ya mashabiki wakiwa katika pich aya pamoja na Mh. Sugu
---
Msanii mahiri wa HIP HOP ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Mr II' a.k.a Sugu, jana alizikonga nyoyo za mashabiki wake waliofurika ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa kufanya makamuzi ya hatari katika tamasha la Usiku wa Sugu. Sugu alisindikizwa na Juma Nature, Profesa Jay, Vinega, Mkoloni na wengineo wengi kwenye shoo hiyo iliyokuwa ya aina yake.
Comments
Post a Comment