MGOMO WA WALIMU WAANZA NA HIVI NDIVYO HALI ILIVYO KUWA KWA BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI JIJINI DAR...!!!

Shule ya msingi Makumbusho, Dar

 Wanafunzi wakiwa wamezagaa nje ya shule baada ya walimu wao kugoma mapema leo katika shule ya msingi Makumbusho jijini Dar 
Mwendo kwa wengine ulikuwa ni kucheza bao wakisubiri walimu wao shule ya msingi Makumbusho jijini Dar. Picha na Richard Bukos na Ally Mnally/GPL

Shule ya Msingi Makuburi, Kinondoni Dar

  Wanafunzi wa shule ya msingi Makuburi manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakiwa wameuchapa usingizi baada ya kuchoka kuwasubiri walimu kuja kufundisha bila mafanikio, wiki iliyopita Chama cha Walimu CWT kilitangaza kuwa leo jumatatu walimu wa shule za Sekondari na Msingi wangeanza mgomo nchi nzima kutokana na kutofikia muafaka kwa madai yao dhidi ya Serikali.

Shule ya Msingi Mabibo, Dar

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mabibo iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa wamelala baada ya kuchoka kuwasubiri walimu kuja kuwafundisha madarasani.

 Ujumbe huoooooooo nao wanaandamana kupinga mgomo wa walimu. Haijajulikana hawa wanafunzi ni wa shule gani.
Wanafunzi wengine wlionekana barabarani Maandamano ya kupinga mgomo wa walimu wao, kitu ambacho ni hatari sana kwa maisha ya watoto hawa na nani wakulaumiwa juu ya hili??? Haijajulikana hawa wanafunzi ni wa shule gani. 
---
Nini maoni yako kuhusu huu mgomo wa walimu?

Picha: Richard Bukos na Issa Mnally/GPL, Full Shangwe Blog, Nkromo blog

Kama una picha za matukio mbali mbali au habari yeyote usisite kutumia kupitia jestinageorge@gmail.com

Comments