Ndugu zangu,
Jana hapa Bagamoyo nikiwa kwenye baraza ya nyumba ya jirani , nilipitisha macho juu ya mpapai. Hapo nikaliona papai limeiva haswa. Nilikaa kimya.
Jana hapa Bagamoyo nikiwa kwenye baraza ya nyumba ya jirani , nilipitisha macho juu ya mpapai. Hapo nikaliona papai limeiva haswa. Nilikaa kimya.
Leo jioni jirani kaja na kunigongea mlango, ananiambia; " Lile papai limeanguka , nimeona heri nikuletee!".
Tafsiri yangu; jirani kanisusia papai. Na dunia hii mengine si ya kuyasusia, maana ni matamu!
Asiyejua maana haambiwi maana, tafakari!
Maggid,
Bagamoyo.
Comments
Post a Comment