Jumuiya ya Watanzania wa Wichita, Kansas, nchini Marekani (TAWICHITA), inasikitika kutangaza kifo cha mtanzania ndugu Martin Phiri kilichotokea Julai 22, Wichita, Kansas.
Baba mzazi wa marehemu Philemon Phiri ameshawasili Wichita, Kansas na mipango ya maziko inaendelea. Taarifa kutoka kwa mke wa marehemu zinasema, marehemu alikutwa na mauti usingizini.
Marehemu ameacha mke na mtoto mmoja. TAWICHITA inawaomba Watanzania wote wanaoishi nchini Marekani na duniani kote kuweza kutoa msaada wao ili kufanikisha mpendwa wetu akapumzishwe katika nyumba yake ya milele.
TAWICHITA imefanya harambee kwa siku za Jumanne na Jumatano, na vilevile harambee hiyo itaendelea tena siku za Ijumaa na Jumamosi. Kwa walio nje ya Wichita, Kansas, wanaweza kuchangia kupitia mfuko maalum unaoitwa "Martin Phiri Fund," kupitia Bank of America.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati katika kufanikisha kupumzishwa kwa mpendwa wetu Martin Phiri. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Amina!
Comments
Post a Comment