DIAMOND AFUNGUKA NA KUELEZEA SABABU ZA MADANSA WAKE KUBAKI MAREKANI...!!!

Wasafi aka Dancers wa Diamond ndani ya Marekani
  Hivi karibuni Diamond Platnumz alipata ziara ya nchini marekani Washington DC kwa kufanya show yake na kwa sasa masnii huyo amesharejea Tanzania lakini madancer wake bado wanakula bata nchini marekani, kitu ambacho kimezua maswali mengi kwa wapenzi na mashabiki wa Diamond. Kutokana na maswali hayo mengi Diamond Platnumz  ameamua kufunguka kupita tovuti yake na kuandika kifuatacho:

Diamond - "NAPATA MASWALI MENGI KUHUSIANA NA DANCERS WANGU KWAMBA JE SIPO NAO TENA?"
 "Jibu ni hapana,nimeamua kuwaacha marekani kwa ajili ya mapumziko ya muda mfupi.Ili waweze kurefresh akili na miili yao kwasababu kiukweli wamefanya kazi kubwa kwa muda mrefu na iliyozaa matunda makubwa...hivyo kwa upendo na Heshima yangu kwao nikaona ni vizuri niwazawadie Mapumziko hayo Nchini AMERICA..... mbali na hayo kuna kingine kikubwa ambacho soon ntawajuza nini wanakifanya pia huko America ili wakirudi wazidi kuleta revolution katika Industry hii ya Muziki Africa."

Comments