MCHUNGAJI AMTABIRIA NEY WA MITEGO KIFO CHAKE NA KUDAI KWAMBA ATAKUFA KWA KUCHOMWA KISU AU KUPIGWA RISASI...!!!
Mtu anayejiita mchungaji hivi karibuni amemtabiria kifo cha rapper Ney wa Mitego kwa kudai kuwa atafariki kwa kuchomwa na kisu au kupigwa risasi.
Ney amesema mchungaji huyo alimfuata nyumbani kwake na mpaka picha zake anazo.
“Nilimrekodi pia, alikuwa anaongea kwa confidence sana, lakini mimi sitishiki na wala siogopi, mimi namtegemea mwenyezi Mungu. Hiki ninachokifanya ni kipaji cha pekee na hawajui kwanini najiamini na siwezi kuacha kukifanya hiki,” Ney alikaririwa jana Jumamosi kwenye kipindi cha Tagz Weekly cha DTV.
Ney amesema mtu huyo alimwambia kuwa ameoneshwa na mwenyezi Mungu, kwamba yeye ni nabii na ni lazika amfikishie ujumbe huo.
“Mwanzo alifika home, aliwakuta wadogo zangu, mimi nikasema amekuja from nowhere siwezi kuongea naye, alianza kuongea na madogo, akawaambia anataka kuonana na Ney mwenyewe, nikawaambia mwambie aondoke.
Nikaona haina haja kwanini nisionge naye, aliacha namba za simu, dogo akampigia akarudi, kurudi ndio akaongea aliyokuwa anaongea.”
”Watanzania wajue kuwa wameanza kutokea watu ambao wanatabiri kifo changu ila nawaambia mimi najua siku yangu ya kufa labda wao waendelee kufanya harakati zao ili kunifelisha na hawawezi kunifelisha, mwenyezi Mungu ndio anajua mimi nafanya nini na wapi ambapo ntaishia.”
“Nilishawaahidi watanzania kwamba huu ni muziki wangu na hii ndio hip hop na hizi ndio harakati ambazo natakiwa kuzifanya,”aliongeza.
Pia amesema siku za hivi karibuni amekuwa akipokea meseji za vitisho kutoka kwa watu wanaomtishia kumuua.
How comes he knows when he is going to die? from what i know only those who have sold their souls to the Devil in exchange of Fame and Fortune knows when they are going to die(artificial Dearth). so that is to say Neema wa mitego(Ney) is just a body without a soul, u see in this world u just can't be a superstar overnight it's very hard that's why these wicked Human beings has chosen the dark side of life (witchcraft) that's why most of them (almost 80%) has no good end in life (they normally die tragically)when their contract with the devil (Baphomet) ends..http://www.jesus-is-savior.com/Evils%20in%20America/devils_music_no_effect.htm
ReplyDelete