MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN DAUDI MWANGOSI AFARIKI DUNIA KATIKA VURUGU ZILIZO JITOKEZA KATI YA POLISI NA WANACHAMA WA CHADEMA MUFINDI MKOANI IRINGA...!!!

 Hayati Daudi Mwangosi
  Pichani Daudi Mwangosi (mwenye kamera) akiwa kazini muda mfupi kabla kufikwa na mauti yake. 
---
Picha na habari na  Francis Godwin.

Mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Mpiganaji Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisi  na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo.

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo  huku askari mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yalipigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini na kudai kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu  magari kadhaa yameharibiwa huku watu kadhaa wakiwa wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi wa NIPASHE.

Habari zaidi zitawajia kadri zitakavyopatikana. JG BLog inaungana na ndugu, jamaa, marafiki na wapiganaji wa Iringa kuomboleza na kulaani kifo cha Mpiganaji Mwangosi. 
Mola aiweke roho yake mahali pema peponi - AMINA

Angalia Video na habari ya vurugu hizo hapa chini:

Comments