Usiku wa kuamkia leo Septemba 26, 2012 ofisi za Jumuiya ya watanzania nchini Ugiriki ziliharibiwa vibaya na baadhi ya watu kujeruhiwa. Licha ya kuwepo kwa Polisi bado walishindwa kuzuia tukio hilo na kuonekana polisi wakiwapa mgongo kabisa Watanzania baada ya hapo walielekea maeneo mengine ya mabaa ya wageni yaliyopo karibu na kuharibiwa vibaya pia.
Sehemu ya uharibifu uliofanywa na wavamizi hao huko Ugiriki usiku wa kuamkia leo
Baadhi ya wadau wakiwa nje ya ofisi za jumuiya ya watanzania wakisahngaa yaliyotokea
Inasemekana ni chama cha XRISI AVGI au Golden down (Neo Nazi) wakiongonzwa na wabunge wao, ndo kimeanza kupiga piga sehemu wanazo miliki na kutembelea wageni ambapo polisi inashindwa kuingilia kati.
Comments
Post a Comment