 |
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mwanza (MPC) Deus Bugaywa akisoma barua ya zuio la polisi kufanyika kwa maandamano hayo ya wanahabari kwa jiji la Mwanza ili kupisha ziara ya Waziri Mkuu sababu ambazo hazikuafikiwa na waandishi wote nao wakaendelea na zoezi la kuandamana kutoka Viwanja vya Ghand Hall jijini Mwanza na kupita barabara kadhaa hadi uwanja wa Nyamagana jijini hapa. |
 |
Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini September 2, 2012 katika mikono ya polisi waliokuwa katika kazi maalum huko Nyololo, Iringa. |
 |
Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza (MPC) kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha kinyama cha mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi akiwa mikononi mwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa.
|
 |
"BAADA YA MWANGOSI NANI ATAFUATA?" Mauaji ya Mwangosi yamebadili sura ya Tanzania kimataifa kuwa ni kisiwa cha amani na sasa kuwa ni kisiwa cha mauaji, kwani Mwangosi amekuwa ni mwanahabari wa 38 kufa akiwa kazini kuanzia mwezi Januari 2012 hadi September 2012 Duniani, na haya ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi kufa akiwa kazini. |
 |
MWANGOSI YOU DIED SERVING THE NATION (Mwangosi umekufa ukilitumikia taifa) Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti katika kijiji cha Nyololo, Mufindi alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa kikatili. |
 |
WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA TUNAJIULIZA:- Kwa nini askari polisi wamegeuka kuwa wauaji? Nani amewatuma polisi kufanya mauaji? Kwa nini wanafanya hivyo hawachukuliwi hatua? Ni nani anayewafanya polisi wawe juu ya sheria? |
 |
Dakika moja ya ukimya kwa waandishi ....... ndani ya uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza |
 |
SOTE TUNALAANI!! |
Tamko la MPC kulaani mauaji ya mwandishi Mwangosi likisomwa na Deus Bugaywa.
 |
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mwanza (MPC) Deus Bugaywa akitoa tamko. (Picha na Mashaka Baltazar, GPL MWANZA) |
Comments
Post a Comment