- TIGO AMERICAN GARDEN KUPAMBA 'HAPPY BIRTHDAY' YA MWANDISHI ANDREW CHALE.
Na Mwandishi wetuKAMPUNI ya Tigo Tanzania leo inatarajiwa kumfanyia sherehe maalum ya siku ya kuzaliwa, mwandishi na mwanahabri wa JG Blog Team mate na wa Tanzania Daima Andrew Chale atakayejumuika na watoto mbalimbali wakiwemo wale wanaoishi kwenye mazingira magumu ndani ya viunga vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Tanzania Daima, Benny Lutaba kutoka kampuni hiyo ya mawasiliano, alisema waliendesha shindano la ‘Sheherekea na Tigo’ kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, kwa wateja wa Tigo nchini, na Chale kufanikiwa kushinda nafasi ya pili kati ya washiriki zaidi ya 30, hivyo kubahatika kufanyiwa sherehe hiyo maalum.
“Wateja wetu wa Tigo waendelee kutuunga mkono, kwani kuna vitu vingi sana katika kusaidia jamii, ikiwemo hii ya ‘Sheherekea na Tigo’ na washindi mbalimbali wanabahatika kujumuika kwa pamoja na familia zao kusheherekea pamoja,” alisema Lutaba.
Kwa upande wake, Chale alisema kuwa, sherehe hiyo anatarajia kufurahia na watoto mbalimbali, wakiwemo wale waishio kwenye mazingira magumu kutoka vituo mbalimbali kama Mitindo House, Umra, Dogodogo Center Kigogo na watoto wa majumbani, wakiwemo wa marafiki zake.
Aidha, Chale alisema kuwa, watoto hao watabahatika kutembelea sehemu mbalimbali ndani ya Nyumba hiyo ya Makumbusho na Utamaduni, kujifunza mengi pamoja na kupata zawadi mbalimbali kutoka kwa American Garden ambao watajumuika nao kwenye viunga hivyo vya Makumbusho.
Shindano hilo lilikuwa maalum kwa ajiri ya wateja wa mtandao wa Tigo waishio jijini Dar es Salaam, ambako walikuwa wakihitajika washindi sita.
JG Blog inapenda kumtakia mwanahabri wetu heri ya siku ya kuzaliwa na maisha marefu yenye afya tele. God bless you Andrew.
Comments
Post a Comment