MKUNGA WA JADI HUKO MBEYA AWASAIDIA WANAWAKE WAJAWAZITO KUJIFUNGUA, LICHA YA KUWA NA UHABA WA VITENDEA KAZI...!!!

  Mkunga wa Jadi Bi Agripina Namwichi (37) (kulia) akimkabidhi mtoto wa kiume Bi Shija Bundala (26) mkazi wa Kijiji cha Mbuyuni, Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya mara baada ya kujifungua salama mtoto wa kiume nyumbani kwa mkunga huyo. Awali mwanamke huyo amewahi kujifungua watoto kwa awamu mbili kupitia Oparesheni katika Kituo cha Afya cha Mbuyuni lakini kwa mkunga huyo inadaiwa alijifungua salama salimini licha ya kuwa na uhaba wa vifaa na eneo maalufu la kitaalamu.
  Mkunga akiandaa eneo la akina mama wajawazito kwa ajili ya mapumziko kabla ya kujifungua.
 Mkunga akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.
Mandhari au sehemu ya kupumzikia akina mama wajawazito ambao hufika kwa mkunga kwaajili ya kujifungua.(Picha zote na Ezekiel Kamanga,Chunya)
Mkunga Bi Agripina akiangalia orodha maalumu ya watoto waliozaliwa katika kituo chake,ambapo zaidi ya watoto 187 wamezaliwa kwa mwaka 2012.
Chumba maalumu kwa ajili ya kijifungulia (labor)
---
NB;- Changamoto ambazo huwabiliwa nazo ni pamoja kuvuja kwa chumba cha kuzalia hususani katika msimu wa masika, uhabawa vifaa vya kuzalishia,v itanda na magodoro na hakuna tozo yoyote ambayo huwadai akina mama wajawazito.

Habari hii ni kwa hisani ya Chimbuko Letu Blog

Comments

  1. Jamani Mungu ambariki huyo mkunga kwa kujitolea kuwasaidia hao wamama kwa kweli.....

    ReplyDelete

Post a Comment