VODACOM FOUNDATION YAENDESHA KAMBI YA MATIBABU MKURANGA...!!!


Mkuu wa kitengo cha Vodacom foundation akizungumza na wakina mama wa wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, waliojitokeza kupata matibabu katika kambi maalum iliyoadhiliwa na Chama cha madaktari wanafunzi Tanzania, na kufadhiliwa na Vodacom Foundation.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wakisubiria kupata huduma za matibabu katika kambi maalum iliyoandaliwa na Chama cha Madaktari Wanafunzi Tanzania, na kufadhiliwa na Vodacom Foundation. Matibabu hayo yalitolewa bure kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Mmoja wa wakazi wa wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani akipimwa uzito na urefu, katika kambi maalum ya utoaji wa huduma za afya iliyoandaliwa na Chama cha Wanafunzi madaktari na kufadhiliwa  na Vodacom Foundation, Mamia ya wakazi wa wilaya hiyo walitibiwa na kupata ushauri wa afya bure. 
Mmoja wa wakazi wa wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani akijiandikisha kupata huduma za Afya, katika kambi maalum ya utoaji wa huduma za afya iliyoandaliwa na Chama cha Wanafunzi madaktari na kufadhiliwa  na Vodacom Foundation, Mamia ya wakazi wa wilaya hiyo walitibiwa na kupata ushauri wa afya bure. 
Mmoja wa wakazi wa wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani akijiandikisha kupata huduma za Afya, katika kambi maalum ya utoaji wa huduma za afya iliyoandaliwa na Chama cha Wanafunzi madaktari na kufadhiliwa  na Vodacom Foundation, Mamia ya wakazi wa wilaya hiyo walitibiwa na kupata ushauri wa afya bure. 
---
Mkuranga, Katika jitihada za kuboresha upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo ya vijijini. Vodacom foundation imeendesha kambi ya matibabu kwa wakazi wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Wakazi hao wamepata huduma za afya bure, na ushauri katika kambi hiyo. Ushauri kuhusu masuala ya huduma za uzazi wa mpango pia zilitolewa.

Kambi hiyo ya afya ni katika mpango ambao utaiwezesha Vodacom Foundation kushirikiana na Chama cha Wanafunzi Madaktari Tanzania ambao watatoa utaalamu na matibabu, Kipindi cha njia panda cha Clouds FM, mabalozi wa afya na taasisi binafsi zinazoshughulikia masuala ya Afya.

Wakati wa kambi hiyo ya Afya, matibabu ya magonjwa mbalimbali yatatolewa na kwa wagonjwa watakao hitaji mahitaji makubwa watapewa rufaa ya kuwawezesha kupata matibabu hayo.Akizungumza katika Kambi hiyo Wilayani Mkuranga, Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule alisema, Mfuko wa huduma za jamii wa Vodacom umedhamiria kufanya kazi na jamii ya Watanzania katika kuboresha maisha yao.

"Kupata huduma za matibabu imekuwa changamoto kubwa nchini. Vodacom Foundation imeshirikiana na sekta binafsi na za umma katika jitihada za kukuza upatikanaji  wa huduma za Afya kupitia kambi za matibabu. Na kusaidia katika ujenzi na vituo vya Afya," alisema Mwakifulefule, na kuongeza kuwa , "Kupitia jitihada hizi za Vodacom Foundation, maelfu ya wananchi watapata matibabu."

Katika mwaka wa fedha wa 2011/2012, Vodafone Foundation ilitengwa ruzuku ya Tsh 114,500,000 kwa Vodacom Foundation, kwa ajili ya kuendeleza miradi ya afya katika maeneo ya vijijini.

Comments