Katika pita pita zangu facebook nimekutana na hii picha ya BOB JUNIOUR RAIS WA MASHAROBARO akiwa amevalia kiharusi zaidi huku pembeni yake kuna mrembo ambaye inasemekana ni mke wake ambaye anatokea Zanzibar na pia hiyo ndoa imefungiwa huko huko Zanzibar. Anyway kama ni kweli hongera zao na tunawatakia ndoa njema na kama ndo zile video zao basi kazi ipo maana naona imekuwa trend ya wanamuziki sasa kushoot video kama vile wanaoa na kuolewa kama vile tulivyo report hapo awali na kuweka picha za Shilole akiwa amevalia nguo ya harusi huku ikiwa ana shoot video ya wimbo wake unao enda kwa jina la DUDU.
Comments
Post a Comment