WALTER CHILAMBO ndiye mshindi wa Shindano la Epic Bongo Star Search (EBSS) 2012. Kufuatia matokeo hayo Kalambo amejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania kutoka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel.
Chilambo ametwaa ubingwa huo baada ya kumwangusha mwana dada kutoka Zanzibar ambaye alikuwa ni mshindani wake wa karibu katika kinyang’anyoro hicho Salma Yusufu.
Pichani ni Walter akiwa anakabidhiwa kitita chake cha milioni 50 mara baada ya kuibuka mshinidi wa EBSS usiku wa kuamkia leo
Walter akiwa anaperform live kwenye finali za EBBS ambao aliibuka mshindi
Salma Yusufu
Shindano la EBSS usiku huu limefikia patamu baada ya washiriki 3 walio ingia katika fainali hizo kutoka na sasa kubakia washiriki wawili ambao ni Walter Chilambo na Salama Yusufu mwakilishi pekee kutoka kisiwani Zanzibar.
Washiriki waliotoka usiku huu na kuachia kitita chaa Shilingi Milioni 50, kikiwaniwa na Walter na Salama ni pamoja na Nsami Nkwabi, Nshoma Ng’hangasamala Wababa Mtuka.
Shindano la EBSS linafikia tamati yake usku huu katika ukumbi wa Diamond Jublee linapoendea kufanyika.

Kama kawaida nao hutoa burudani ....Chief Jaji na mratibu wa Shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS), Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, Ritha Poulsen a.k.a Madam Ritha, akifurahia jambo wakati washiriki wakitumbuiza jukwaani. Kulia ni Jaji mwingine Master Jay akionekana kama kukera na kicheko cha Madam Ritha.

Mashabiki na wapenzi wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) waliofurika katika ukumbi wa Diamond Jubelee wakilipuka kwa shangwe baada ya mmoja wa washiriki ambao wanamkubali kumaliza kufanya show yake.


Huyu ni Salama Jabir na hapa ni katiak yale ya Look ndani ya fainali za EBSS 2012

Washiriki wa Washindano la EBSS 2012 ambao wamefanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa kuanza kwa fainali hizo. Ni ndani ya Ukumbi wa Diamond Jijini Dar es Salaam. Mshindi kuondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania.

Shindano la kutafuta vipaji la EBSS 2012 linataraji kufanyika usiku huu kuanzia majira ya saa 3:00 na kwa mujibu wa waandaaji litakuwa likionekana LIVE kupitia Luninga zenu hasa kupitia ITV. Father Kidevu Blog nayo itawapa yale yanayojiri katika tukio hilo.

Hawa ndio washindani je nani ataibuka mshindi na kuondoka na Milioni 50 usiku huu. Fuatalia zaidi tutakujuza.
Source: Mroki M
Comments
Post a Comment