WAZIRI WA MAJI MHESHIMIWA JUMANNE MAGHEMBE ATUA NCHINI UINGEREZA KWA ZIARA YA KIKAZI YA WIKI MOJA...!!!

Mheshimiwa Balozi Kallaghe, alitumia fursa hiyo kumfahamisha Mhe. Waziri Maghembe maendeleo ya kazi za Diplomasia ambazo Ubalozi unafanya kwa niaba ya serikali nchini Uingereza. Kwa upande wake Mheshimiwa Waziri Maghembe, alielezea mafanikio ya serikali katika kuwapatia wananchi huduma ya maji na juhudi zinazoendelea kufanywa kuondoa tatizo la Maji na kuhakikisha tatizo hilo linakuwa historia nchini Tanzania.
Waziri Maghembe anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na viongozi wakuu wa sekta ya Nishati na Maji nchini Uingereza yenye lengo la . Aidha ujumbe huo wa Tanzania, ukiongozwa na Mheshimiwa Waziri Maghembe utamaliza ziara yake nchini Uingereza siku ya Alhamis, tarehe 29 Novemba 2012.
Mheshimiwa Waziri Maghembe, pamoja na Mheshimiwa Balozi Kallaghe, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na baadhi ya Maofisa wa Ubalozi hapa London.
Comments
Post a Comment