Habari zenu nyote wapenzi wa muziki wetu Mimi AT kupitia hii blog www.jestina-george.com ni xclsv ni kwamba mwanzoni mwa Mwaka kesho nitatoa wimbo mpya mahsusi kwa wale wenye choyo, kijicho, husda, togoo, nogwa, maneno maneno, wambea, roho chafu, kibri, ngebe, majigambo, hasira za kitamaa, wababaifu malaghai, rogi rogi, nk iyo nyimbo itawahusu maana mkemeaji hakuna na mm nimejitolea kua zaidi ya chuo cha mafunzo ili walibaki waishi kwa Amani baada ya Dharuba hi kuwafikia walengwa wimbo huo nimetengeneza NK Production chini ya Criss na Video itafanywa na Kwetu Studio.
---
Baadhi ya maneno katika wimbo huo wa "HANA HAYA."
"Kama unataka vita lazima ujiandae, mjini umenikuta kiasi unishangae, Mimi na ww hatuendani katafute kibanda ukalale, Mimi ni mwema ww ni Jini kazi yako kujichanja Machale, Ukinitazama ninavyo vutia roho inakuuma unanichuria, ukinitazama ninavyo nukia roho inakuuma unanichuria, Hawa ndio wale walikuja mjini hawana la kufanya Hawa ndio wale kazi yao kugombania tu Mabwana..!!
Kaeni mkao wa kuburudika.....
Comments
Post a Comment