MH. GODBLESS LEMA ASHINDA RUFAA NA KURUDISHIWA UBUNGE WAKE LEO...!!!


Mbunge wa Arusha Mjini-CHADEMA,Mh Godbless Lema akitoa hotuba fupi mara baada ya kushinda katika rufaa ya kesi yake ya kupinga matokeo, iliyosomwa jijini Dar es Salaam leo kulia kwake ni Mbunge wa Chadema Arumeru Mashariki Joshua Nasari
Mbunge wa Arusha Mjini-CHADEMA,Mh Godbless Lema akiondoka kwa staili ya maandamano Mahakamani leo baada ya kushinda katika rufaa ya kesi yake ya kupinga matokeo, iliyosomwa jijini Dar es Salaam leo kushoto kwake ni katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na katibu wa kuteuliwa wa kanda maalum ya Dar es salaam Henry Kilewo
  Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Mh Freeman Mbowe(wa pili kulia)akiteta jambo na Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)mH gODBLESS Lema ndani ya mahakama leo asubuhi muda mfupi kabla ya rufaa ya kesi yake ya kupinga matokeo iliyosomwa jijini Dar es Salaam leo kutolea hukumu na kuamuru lema kuwa ni mbunge Halali wa Arusha Mjini wa Pili kushoto ni Mbunge wa Arumeru Mashariki(CHADEMA)Mh Joshua Nasari na wa kwanza kushoto ni katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na katibu wa kuteuliwa wa kanda maalum ya Dar es salaam Henry Kilewo
  Kutoka kushoto ni Mke wa Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Godbless Lema,katibu wa kuteuliwa wa kanda maalum ya Dar es salaam Henry Kilewo,Mbunge wa Arumeru masharii Joshua Nasari,Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe wakiwa mahakama ya rufaa leo asubuhi muda mfupi kabla ya hukumu ya kesi ya kutolea
Mawaikili wakiwa kwenye viti vyao leo muda mfupi kabla ya hukumu ya kesi ya lema kutolewa asubuhi hii
Baadhi ya watu mbalimbali waliofurika mahakamni leo kusikiliza hukumu ya lema
 Wakili Machachari na Mbunge wa Singida Vijijini(CHADEMA) Tundu lissu ambae alikua mtetezi wa Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Godbless lema ambae aliingia kwenye kesi upande wa utetezi baada ya kesi kufika mahakama ya rufaa akiongea machache baada ya hukumu hiyo.watu mbalimbali walimshangiliwa sana leo
  Vitalisi kimomogoro,wakili wa lema.huyu ndiye amekuwa na kesi hii tangu ilipoanza
  Askari wakisindikiza msafara wa wafuasi wa CHADEMA baada ya Mahakama ya Rufaa kutoa hukumu ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (CHADEMA)Godbless Lema.Picha Zote na Habari Kwa hisani Kubwa ya Mjengwa Maggid
--
Hukumu imeangalia haswa swala la Locus Stand ya kama waliofungua kesi walikuwa na haki kisheria ya kufanya hivyo.imeangaliwa kwa kina na kuonekana kuwa kadiri ya pingamizi ya mawakili wa lema kimomogoro na Tundu Lissu,waliofungua shitaka dhidi ya lema hawakuwa na locus stand ya kufanya hivyo.kwa hiyo mengine yote yanakuwa null and void.hukumu haikuchukua hata nusu saa kwa hiyo Mheshimiwa Godbless Lema  lema ni mbunge halali wa arusha mjini kuptia CHADEMA tangia leo

Comments

  1. Nimefurahishwa sana na hukumu hiyo, ntalala ucngz mzuri mm leo

    ReplyDelete

Post a Comment