MKURUGENZI MTENDAJI WA VODACOM RENE MEZA, AHUTUBIA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA JUKWAA LA WAHARIRI NCHINI (TEF) NA KUKABIDHI MISAADA MJINI TANGA...!!!
Mkurugenzi Mtedaji wa Vodacom Rene Meza akihutubia katika mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) mjini Tanga mwishoni mwa wiki. Rene alitumia nafasi hiyo kuzungumzia uwekezaji wa Vodacom hapa nchini na mchango wa kampuni hiyo katika uchumi wa nchi na maendeleo ya ustawi wa Jamii.
Christina Chambo wa Kituo cha Comfort akiongoza sala ya ufunguzi wa hafla ya utoaji zawadi ya Krismasi kwa watoto wa kituo hicho cah Comfort na Diana vyote vya Mjini Tanga vilivyotolewa na wafanyakazi wa Vodacom kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom. Zaidi ya Sh. 50 Milioni zitatumika katika kampeni hiyo na kunufaisha makundi yenye uhitaji sehemu mbalimbali nchini.Meza Kuu kutoka kushoto ni Bi Martha, Yessaya,Rene, Saanani na aliyesimama kulia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzaniia (TEF) Tefil Makunga akimtambulisha Mkurugenzi Mtedaji wa Vodacom Rene Meza (wa pili kushoto) kabla ya Rene kuhutubia mkutano mkuu wa mwaka wa TEF mjini Tanga mwishoni mwa wiki. Rene alitumia nafasi hiyo kuzungumzia uwekezaji wa Vodacom hapa nchini na mchango wa kampuni hiyo katika uchuni wa nchi na maendeleo ya ustawi wa Jamii. Kushoto ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim
Mhariri Mkuu wa Habari wa Channel Ten na Radio Magic FM Benadina Chahali (kushoto) na Mhariri wa gazeti ya Uhuru Lilian Timbuka wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtedaji wa Vodacom Rene Meza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) mjini Tanga mwishoni mwa wiki. Rene alitumia nafasi hiyo kuzungumzia uwekezaji wa Vodacom hapa nchini na mchango wa kampuni hiyo katika uchuni wa nchi na maendeleo ya ustawi wa Jamii.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Comfort wakipokea vifaa vya shule na vyakula kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza huku Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Masoud Saanani, Meneja wa Vodacom Tanga Mjini Edgar Malimbo na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule wakishuhudia.
Rene (mwenye koti jeusi katikati) pamoja na watoto wa kituo cha Comfort wakiwa katika picha ya pamoja na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walioshiriki katika hafla ya ukabidhi zawadi ya Krismasi kwa vituo vya Comfort na Diana vya Mkoani Tanga. Wafanyakazi wa Vodacom wamekusanya kiasi cha Sh. 50 Milioni kusaidia watoto yatima na Makundi mengine yenye uhitaji kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom.
Comments
Post a Comment