KHERI YA KRISMAS
Chama cha Mapinduzi Uingereza kwa niaba ya Watanzania wote waishio hapa Uingereza, tunapenda kuchukua nafasi hii pekee katika kuufunga mwaka, kuwatakia Watanzania wote salaam za kheri ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.
Ni imani yetu kwamba kwa pamoja tunaungana kusherekea Sikukuu hii ya Krismas na kupata fursa ya Kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wale tuliobarikiwa kufikia fursa hii na kuimarisha Upendo na Amani miongoni mwetu sisi sote.
Tunapofikia wakati huu wa sherehe za mwisho wa mwaka, hatuna budi basi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa nafasi yake ya Upendo aliyotupatia na kuwaombea kila mmoja wetu kadri ya hitaji lake na pia kuiombea Serikali yetu nyumbani ili iweze kufikia malengo ya kijamii iliyojiwekea.
MUNGU IBARIKITANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA
Imeandaliwa na Idara ya Itikadi, Siasa na Uenezi.
CHAMA CHA MAPINDUZI
TAWI LA UNITED KINGDOM
21 Desemba, 2012
Comments
Post a Comment