WATANZANIA UK WAMUAGA MAREHEMU MARIAGORETH NDANGIO...!!!

Leo Tarehe 04/12/12 asubuhi muda wa saa tano watanzania waishio Luton Uingereza, Ndugu na marafiki kwa ujumla walijumuika kataka kanisa la Kikatoliki la Holy Ghost  Westbourne Luton Uingereza katika ibada ya kumuaga MariaGoreth tayari kwa safari ya mazishi kuelekea Nyumbani Tanzania.

Katika ibada hiyo mama mzazi wa marehemu aliwashukuru watu wote waliojitoa kwa kila hali wakati wa kumuuguza mwanae mpaka mauti ilipomkuta. Pia kaka wa marehemu alisoma historia fupi ya marehemu na  upendo na ushirikiano alikuwa nao na watu wote.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho Jumatano kuelekea Tanzania kwa ajili ya mazishi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Luton ( Luton Tanzanian Community ) Bw. John Mbwete kwa niaba ya Familia ya marehemu na Jumuiya anatoa shukrani kubwa kwa watu wote waliojitoa kwa hali na mali, ubalozi wa Tanzania UK na Tanzania Association kwa ushirikiano waliotupa katika kufanikisha safari ya mwisho ya MARIAGORETH Kuelekea Tanzania. 

Bwana ametoa na Bwana ametwaa sifa na utukufu kwa Mwenyezi Mungu.

  Shukrani

ABRAHAM SANGIWA

Katibu – Luton Tanzanian Community ( TLC )

Comments