ZIARA YA NAIBU WAZIRI TARIME KUHAMASISHA KUKATAA UKEKETAJI...!!!

 Mhe. Ummy mwalimu akiwa pamoja na Kamishna Msaidizi wa Polisi  na Mkuu wa Dawati la Jinsia la Polisi, Adolphina Chalo, Katibu Tawala Tarime  Erenest Kabohora na Mwenyekiti wa halmashauri Tarime
Mmoja wa wananchi akichangia hoja wakati wa mkutano wa hadhara  kuhamasisha kuacha vitendo vya Ukeketaji

Sehemu ya wanawake waliohudhuria katika mkutano wa hadhara juu ya uhamasishaji  wa kuachana na vitendo vya ukeketaji

 Kundi la Vijana wakisherekea baada ya watoto wa kike kukeketwa
 Kijana wa kiume akiimarisha ulinzi kwa mtoto wa kike ambaye amekeketwa  wakati wa sherehe za Ukeketaji Tarime
Mhe.Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wazee wa mila katika kijiji cha Kiongera, Kamishna Msaidizi ,Katibu Tawala  na Mwenyekiti wa Halmashauri.
---
Pichani ni matukio mbalimbali  kufuatia ziara ya Mhe. Ummy Mwalimu
Naibu Waziri ,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wilayani
Tarime kuhamasisha  wananchi wa Tarime kuachana na ukeketaji  kwa
watoto wa kike. Mhe.Ummy yupo Wilayani hapa kwa ziara ya siku tano
kuhamasisha wananchi kuachana na ukeketaji kwa watoto wa kike. Pamoja
nae ameambatana na Kamishana Msaidizi  Mwandamizi wa Polisi ambaye pia
ni Mkuu wa dawati la Jinsia la Polisi Makao Makuu Adolphina Chalo.

Comments