Elizabeth Michael ‘Lulu’ akishuka kutoka katika gari lililomleta leo Mahakama Kuu wakati wa kukamilisha taratibu za kupata dhamana.
Lulu akiingia Mahakamani huku akisindikizwa na Askari Magereza
Lulu akiingia majengo ya mahakama
Lulu akitoka katika lango Kuu la Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kupata dhamana
Lulu akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa habari waliotala kufanya nae mahojiano mfupi baada ya kupata dhamana.

Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu amechiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda mrefu sana.
Lulu akitokwa na machozi ya furaha
Lulu akiingia kwenye gari
Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
---
Baada ya jana kushindikana kwa sababu zisizo zuilika hatimaye msanii maarufu Elizbeth 'Lulu' Michael ametoka kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yote ya dhamana yake yaliyo tolewa na mahakama kuu.
Mara baada yakutoka Lulu alieyeonekana akiwa mwenye majonizi na furaha kiasi aliomba watanzania wote wamuombee maana hii ni dhamana tu na kesi yake bado inaendela. Ali washukuru watu wote waliokuwa pamoja nae katika mkasa huu na kusema “Nawashukuru watu wote na nilikua naomba watu waendelee kuniombea sababu hii ni dhamana tu lakini kesi bado ina safari ndefu… nawashukuru wale wote waliokua na mimi kwa hali yeyote ile na zaidi zaidi namshukuru sana Mwenyezi Mungu.”
Wakili wake Ndugu Flugence Massawe amesema kwamba hii ni hatua ya kwanza kwasababu case bado inaendelea. Kwa sasa wanasubiri mahakama itoe tarehe ya Lulu kurudi mahakamani.
Msikilize Lulu hapa chini:
mungu akubariki na wote walio kuwa pamoja na dada yuo mungu awabariki na bado tutazidi kukuombeya na wewe usichoke kuomba maana bila yeye yote ya singe honekana
ReplyDeletelulu mungu akubari mpendwa kuwa na amani mahakama imekuachi lala 2
Delete