M-PESA YAAMSHA ARI YA WANANCHI KUKATA BIMA...!!!

Utamaduni wa watanzania kujiunga na huduma za Bima nchini kama njia mojawapo ya kukabiliana na gharama za majanga na matukio mengine ya asili ikiwemo kifo umeaonekana kuongezeka kufuatia kuwepo kwa urahisi wa kukata na kujiunga na bima kupitia simu za mkononi.

Kuongezeka kwa utamaduni huo wa kukata bima kunasaidia kuondokana na dhana ya kwamba kukata bima ni sawa na kujitakia majanga jambo mbalo hata hivyo halina ukweli na badala yake bima imekuwa msaada mkubwa kwa wanajamii katika kumudu gharama zitokanazo na majanga na matukio mengine yasiyoweza kuepukika.

Kuwepo kwa urahisi huo ni matokeo ya ubia wa kibishara kati ya kampuni ya Bima ya Heritage na Kampuni ya Vodacom Tanzania ambapo sasa mteja wa Vodacom ameewezeshwa fursa rahisi na ya uhakika ya kujiunga na huduma za bima kupitia simu za mkononi kutumia huduma ya M-pesa. Hii ni huduma ya kwanza na ya aina yake inayopatiakana Tanzania pekee.

“Tumeshuhudia mageuzi makubwa katika sekta ya bima nchini tangu tulipoanzisha utaratibu wa kukata bima kupitia simu za mkononi huku mteja akifanya malipo ya bima yake kwa njia ya M-pesa, tunaamini ubia huu umekuwa wa faida kubwa kwa jamii.”Amesema  Mkuu wa Kitengo cha huduma za bima wa kampuni ya Heritage Tanzania, Bw. Joseph Mardai.

“Ni wazi sasa upo urahisi na jamii inaanza kuona umuhimu wa bima. Tayari watu kadhaa wameshafanikiwa chini ya mpango huu ambapo kampuni ya Heritage Tanzania imeweza kuwalipa wanufaika wa bima hizo za Upendo na Faraja kiasi cha fedha kusaidia gharama za mazishi kwa urahsi zaidi kupitia M-pesa, hakuna usumbufu wala gharama za ziada.”Ameongeza Mardai.

Mardai amesema mabadiliko ya kifikra yanayoanza kuonekana hivi sasa nchini kuhusu huduma za bima hasa kwa bima zinazohusisha vifo kutasadia kwa kiwango kikubwa namna jamii inavyoweza kuondokana na hofu na mzigo mkubwa wa kugharamia shughuli za mazishi na matibabu.

“Hakuna anaependa kuzungumzia kifo lakini tunapogundua kwamba hakuna mwenye uwezo wa kukizuia wala kutambua ni wakati upi kitamfika ni dhahiri tunapaswa kutafakari namna bora ya kupunguza mzigo kwa familia zetu katika kugharimia shughuli za mazishi.” Amesema Mardai Na kuongeza kuwa “Huduma za Faraja na Upendo inatoa namna bora ya kupata suluhisho.”

Chini ya utaratibu wa ukataji wa bima kwa njia ya M-pesa mteja anaweza kukata na kulipia bima yake wakati wowote na mahali popote na hata kupokea fidia ya malipo ya bima yake pale tatizo lililokatiwa bima linapotokea ambapo fedha hizo hupokelewa na wanufaika aliowaandikisha kwenye mkataba wa bima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema ubunifu katika Vodacom unaendelea kudhihirisha azma ya kampuni hiyo katika kubadil na kurahisisha maisha.

“Tumekuwa na dhamira hiyo ya kuhakikisha teknolojia ya simu za mkononi haishii katika kupiga na kupokea simu au kutuma ujumbe mfupi wa maneno tunataka kuona maisha ya watu yakiwa rahisi na mepesi zaidi kupitia simu zao za mkononi. Huduma hii ya Bima ni uthibitisho mmojawapo wa dhamira inayotuongoza katika biashara.”Amesema Meza.

“M-pesa imeleta mapinduzi makubwa hapa nchini jinsi jamii inayoishi, hatuna sababu yakurudi nyuma tutaendelea kuongoza katika ubunifu na kuziunganisha huduma mbalimbali katika mfumo wa M-pesa ili kuzileta karibu na wananchi.”Alisema Meza na kuongeza “Tayari kwa sasa biashara nyingi zimeshaunganishwa na mfumo wa M-pesa kuanzia usafiri wa anga, malipo kwenye maduka makubwa – Supermarkets, uchangijaji katika mifuko ya hifadhi ya jamii, malipo ya ving’amuzi n.k.” 

Hivi karibuni kampuni ya Heritage ililipa wateja wake wawili wa kwanza kabisa tangu kuanza kwa huduma ya bima kwa kwa njia ya M-pesa.
Wateja hao ni  mke wa Bw. Mathias Mahunda, Bi. Fransisca Mahunda ambae mumewe alikuwa mteja aliyekuwa na Bima ya Upendo aliyefariki dunia Novemba 17, mwaka huu ambae alilipwa kiasi cha sh, milioni mbili.

Mwengine aliyenufaika na bima hiyo ni mke wa marehemu Kulwa Mtangaki, Bi. Julieth Mtangaki, ambaye mumewe marehemu Bw. Mtangaki alifariki dunia Novemba 12 kwa ajali na bima yake ya Faraja iliwezesha mkewe kupewa kiasi cha sh. 200,000 kama kusaidia gharama za Maziko.

Katika hatua nyengine wateja mbalimbali wa Vodacom wamekuwa wakinufaika na huduma za bima kwa kupatiwa Sh. 200,000 kama promohseni ya kufanya miamala kumi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

“Kila mteja wetu anaefanya miamala kumi kwa mwezi tunamzawaidia bima ya Sh. 200,000 katika mwezi unaofuata ambayo hudumu kwa kipindi cha mwezi mmoja na anaweza kunufaika na fidia ya bima iwapo atakutwa na umauti ndani ya kipindi hicho cha mwezi mmoja fedha ambazo hulipwa kwa wanufaika anaowapendekeza.”Alisema Meza
Mteja hupaswa kuandikisha majina ya wanufaika wake kupitia utaratibu unaoelezwa kwenye ujumbe mfupi wa maneno anaotumiwa kujulishwa kuhusu kuingiziwa kiasi hicho cha fedha (200,000) katika akaunti ya bima. 

Comments