"Mabosi wamama nyumbani inabidi tubadilike hivi ndivyo wafanya kazi wa ndani wengi wanafanyiwa na pia hapo ndio ndoa zetu zinapo ingia dosari..... mfano; Dada umeshapika chai? njoo umbadilishe mtoto pampers, hivi jana ulipika maandazi? Nibandikie maji ya kuoga, ninyooshee nguo za kazini, lete kwanza chai, mmh mbona haya maandazi mabaya, mi nitengenezee chapati za maji. He mbona hujafagia nje? Yaan hamna hata kazi iliyofanyika naona unazunguka zunguka tu. Mpikie mtoto mtori leo. Halafu uunge wale samaki na nazi upike na wali. Pia ukumbuke kufua na kufuta vumbi ndani........HII KALI!
Comments
Post a Comment