Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati), Mwakilishi wa ADB Tanzania, Toniya Kandiero, Naibu Waziri wa Mindombinu na Mawasiliano, Issa Haji Gavu, Katibu Mkuu wa Miundombinu ,Mawasiliano,Dk.Juma Malik Akili, na Mkuu wa Mkoa wa Kasakazini Unguja Pembe Juma (kushoto), wakitembea katika Barabara ya Mfenesini-Bumbwini baada ya kufunguliwa Rasmi jana, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Dk.Ali Mohamed Shein na Mwakilishi wa ADB Tanzania, Toniya Kandiero,wakikata utepe kufungua Barabara ya Mfenesini-Bumbwini, iliyojengwa na Kampuni ya Mecco kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana. Barabara hiyo imejenga na Kampuni ya Mecco kwa umefadhili wa na Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi, ikiwa ni shamrashamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Shein, akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja.
Baadhi ya Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, wakimsikiliza Dk. Shein, alipokuwa akizungumza nao katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu

Hiyo Barbara imejengwa kwa ufadhili ya African Development Bank (ADB) Sio Bank ya Dunia. Sijui kwa nini waandishi hawakuwauliza wizara husika.
ReplyDelete