Salam,
Baada ya barafu nyingi kuanguka na kuleta tafrani nchini Uingereza mapema wikiend iliyopita, baadhi ya wakazi wa mji wa Reading badala ya kuendela kulalamikia usumbufu uliotokana na kusitishwa kwa huduma nyeti kama usafiri wa anga, treni, barabara, kufungwa kwa shule, maduka n.k wao hawakulaza damu waliamua kuichangamkia fursa ambayo inatokana na kuanguka kwa barafu.
Fursa hii sio nyingine bali ya kufurahia mchezo wa kuteleza (Bobsleighing) ambao hufanyika kwenye nchi za baridi kama Norway, Canada, Urusi n.k.
Familia mbalimbali zilijitokeza ili kufurahia kwa pamoja.
Asanteni,
Urban Pulse Creative
Hata mbwa hawakuachwa nyuma
Mama na Mwana wako kimichezo zaidi
Snow (theluji) kila mahali
watoto wakijiandaa
michezo ikiendelea
wazee na wajukuu wakijiandaa kupanda kileleni
wadau wakipanda kwenye mwinuko ili kupata kasi ya kuteleza chini
Comments
Post a Comment