WANAMUZIKI WA INJILI WA KIMATAIFA BWANA NA BIBI MBASHA WALIPO TEMBELEA OFISI ZA UBALOZI LONDON NCHINI UINGEREZA...!!!

 Mheshimiwa Balozi, Peter Kallaghe, akipokea zawadi ya CD na DVD kutoka kwa Wanainjili hao Dada Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha. Wanainjili hao wakiwa nchini Uingereza, walitembelea Miji ya Glasgow, Chemsford na Reading.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, akiwa kwenye picha ya pamoja na wanamuziki maarufu wa Kimataifa wa nyimbo za Injili Dada Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha (Kulia), Askofu Ernest Irungu, ambaye ni Kiongozi wa nyimbo za Injili na ni Mkuu wa Chuo cha Vision College of Theology kilichopo London, Uingereza, mama Zest Irungu (mke wa Bishop Irungu) na Bibi. Mwambola, walipotembelea Ofisi za Ubalozi jana. Bwana na Bibi Mbasha wapo nchini Uingereza, wakitokea Amerika kujitangaza na kutangaza Injili.


Comments