MWANAMITINDO MILEN MAGESE ACHANGIA MILIONI 15 KUSAIDIA ELIMU MKOA WA MTWARA...!!!

Millen akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mara baada ya kuwasili mkoani hapo kwenye tour yake ya Millen Magese Foundation Tanzania
Millen akiongea machache na wadau pamoja na mkuu wa mkoa wa Mtwara nje ya ofisi zao mkoani humo

Mhe. Sophia Simba pia alikuwepo na ni baada ya miaka 12 wameweza kuonana tena na Millen

Mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese alipowasili mkoani Mtwara kwenye tour yake ya Millen Magese Foundation
Millen akisign kitabu cha wageni

Mkuu wa Wilaya akimshukuru Millen baada ya kupokea hundi ya milioni 15 ambazo zitasaidia katika Elimu wilayani humo
Millen akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Serikali mkoani Mtwara.

Picha zinazo fuata nimeacha caption alizo weka Millen maana zinajielezea vizuri zaidi







Kutoka Mtwara:
MWANAMITINDO mahiri wa kimataifa ambae pia aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2001 Millen Magese juzi alitoa milioni 15 kusaidia elimu kwa shule ya msingi ya Mjimwema na Lilungu za mkoani Mtwara.

Millen alikabidhi msaada huo kwa wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Willman Ndile huku akishuhudiwa na Mbunge wa Mtwara mjini Hasein Murji pamoja na wadau wengine wa maendeleo mkoani humo.

Millen akikabidhi hundi ya milioni hizo 15 baada ya kutembelea shule hizo na kujionea hali hali ilivyo alisema kuwa msaada huo ni kutimiza ahadi yake aliyoiweka siku moja angeenda mkoani humo na kusadia masuala ya elimu.

Awali akitembelea shule ya Mji Mwema iliyopo kata ya Magengeni aliikuta shule hiyo ikiwa katika hali duni ambapo kuna vyumba viwili vya udongo vya madarasa huku kukiwa na wanafunzi wengi zaidi.

Millen aliwaambia wazazi pamoja na wanafunzi waliokuwa katika shule hiyo kuwa ameguswa na namna ambavyo hali ni mbaya katika eneo hilo na kuongeza kuwa yupo tayari kuwa mlezi wa shule hiyo.

Alisema kuwa ili wanafunzi waweze kusoma na kufikia malengo yao wanatakiwa kusoma katika mazingira bora na yenye kuvutia ambapo alisema kuwa ni jukumu lake kuonesha mfano katika hilo.

Aliwasihi wazazi pamoja na wakazi wa eneo hilo kuhakikisha kuwa wasaidia katika ujenzi wa shule hiyo kwa kujitolea kwa hali na mali kufanikisha ujenzi huo.

“ Iwapo mkisaidi kuleta mchanga wengine wakafyatua matofali basi kila kitu kitaenda sawa na tunaweza kujenga madarasa bora zaidi” alisema Millen.

Alisema kuwa kwa sasa ameamua kuanzisha Taasisi yake iitwayo Happiness Millen Magese Foundation  kusaidia masuala mbalimbali kama vile elimu, jinsia na harakati za maendeleo ya akimama.

Naye Mbunge wa Mtwara mjini  Hasein Murji alihamasika zaidi na kuahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi zaidi wa shule hiyo.

Alisema kuwa kwa muda mrefu alikuwa akiumiza kichwa kutafuta namna ya kusaidia kujenga shule hiyo na kwa msaada huo wa Millen ni hatua kubwa kwa maendeleo ya shule hiyo ya Mjimwema.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Willman Ndile aliwataka wananchi kuhamasika zaidi kwa kuunga mkono harakati za Millen katika kuimarisha elimu mkoani humo kwa kuwa ameonesha mfano mzuri akiwa kama mwanamitindo.

Pia millen alimkabidhi mkuu huyo wa wilaya milioni tano kwa ajili ya ununuzi wa madawati ya shule ya msingi Lilungu iliyopo kata ya Ufukoni Mtwara mjini.
Mwisho

Picha na habari kwa hisani ya Elimu Bora Tanzania Blog na Millen Magese Instagram

Comments