NAIBU WAZIRI WA ELIMU PHILIP AUGUSTION MULUGO ATOA KALI NYINGINE NA KUSEMA " HAJUI LOLOTE KUHUSIANA NA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA INAYOENDELEA"...!!!

Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, naibu waziri wa elimu katika serikali JK ametoa mpya ya kufungua mwaka baada ya kuulizwa juu ya maendeleo ya mitihani ya kidato cha sita iliyoanza leo. Alipoulizwa na kituo cha EATV kupitia kipindi cha HOTMIX, waziri huyo mwenye historia ya kutofahamu vyema historia ya nchi yake alitoa jibu kuwa.....

"Sina taarifa yoyote kuhusiana na kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita, kwasasa nipo kwenye kikao cha NEC, labda waulizeni waliopo DSM ofisini. Alipoulizwa zaidi aliendelea kusema mimi sijui kuhsuiana na mitihani ya kidato cha sita. Huyu ndie Naibu waziri wa elimu ndugu Mulugo."

Hivi huyu waziri bado yupo tu na anaangaliwa aisee ni aibu kubwa sana I hope atashughulikiwa.

Comments