BANDARI YAISAMBARATISHA FALCON MABAO 2-0 KATIKA MPAMBANO WA LIGI KUU YA GRAND MALT YA ZANZIBAR ULIYO FANYIKA UWANJA WA AMAAN MJINI ZANZIBAR JANA...!!!

Rashid Omar wa Bandari (kulia) akichuana na Rajabu Mlindwa wa Falcon, kwenye uwanja wa Amaan jana.
Rajabu Mlindwa wa Falcon (kushoto) akijaribu kumpita Rashid Omar wa Bandari.
Rajabu Mlindwa wa Falcon akimtoka Rashid Omar wa Bandari.
Mohamed Hassan wa Bandari (kushoto) akituliza mpira mbele ya Ali Suleiman wa Falcon.
Mlinzi Rashid Omar wa Bandari (kulia) akimzuia mshambuliaji wa Falcon, Mbarouk Marshed
asiende na mpira.
Wachezaji wa Bandari na Falcon wakigombea mpira kwenye pambano lao la ligi kuu ya Grand Malt ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amaan jana.
Mchezaji wa Falcon (kulia) akimkwatua mshambuliaji wa Bandari.
Wachezaji wa Bandari na Falcon wakikimbia kuuwahi mpira.
Picha zote na Martin Kabemba.
Hivi siku hizi washabiki wa mpira wa team zetu hakuna au ni vipi? Maana ukiangalia hapa utasema wako mazoezini????? Jamani tusupport michezo yetu na wachezaji wetu pia.

Comments